Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 42 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَأَخَذۡنَٰهُم بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَتَضَرَّعُونَ ﴾
[الأنعَام: 42]
﴿ولقد أرسلنا إلى أمم من قبلك فأخذناهم بالبأساء والضراء لعلهم يتضرعون﴾ [الأنعَام: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tuliwatuma, ewe Mtume, Wajumbe kuwaendea makundi ya watu kabla yako kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakawakanusha na tukawapa mtihani katika mali yao, kwa ufukara mwingi na dhiki za maisha, na tukawapa mitihani katika miili yao, kwa magonjwa na kuumwa, ili wajidhalilishe kwa Mola wao na wanyenyekee Kwake Peke Yake kwa ibada |