Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 45 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْۚ وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[الأنعَام: 45]
﴿فقطع دابر القوم الذين ظلموا والحمد لله رب العالمين﴾ [الأنعَام: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watu hawa walimalizwa na kuangamizwa walipomkanusha Mwenyezi Mungu na kumkanusha Mtume Wake; hakuna yoyote aliyesalia kati yao. Shukrani na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Muumba na Mwenye kumiliki kila kitu, kwa kuwapa ushindi mawalii Wake na kuwaangamiza maadui Zake |