Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 46 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمۡعَكُمۡ وَأَبۡصَٰرَكُمۡ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِهِۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ هُمۡ يَصۡدِفُونَ ﴾
[الأنعَام: 46]
﴿قل أرأيتم إن أخذ الله سمعكم وأبصاركم وختم على قلوبكم من إله﴾ [الأنعَام: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Nambieni ikiwa Mwenyezi Mungu Ameyaondoa masikizi yenu Akawafanya viziwi, Akayaondoa macho yenu Akawafanya vipofu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu mkawa hamufahamu neno, basi ni mola gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, awezaye kuwarudishia nyinyi vitu hivyo?» Angalia, ewe Mtume, ni namna gani sisi tunawatolea hoja aina mbalimbali, kisha wao baada yake wanakataa kukumbuka na kuzingatia |