Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 53 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لِّيَقُولُوٓاْ أَهَٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنۢ بَيۡنِنَآۗ أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَعۡلَمَ بِٱلشَّٰكِرِينَ ﴾
[الأنعَام: 53]
﴿وكذلك فتنا بعضهم ببعض ليقولوا أهؤلاء من الله عليهم من بيننا أليس﴾ [الأنعَام: 53]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hivyo basi Mwenyezi Mungu Amewapa mtihani waja Wake kwa kutafautiana mafungu yao ya riziki na umbo, Akawafanya baadhi yao matajiri na wengine maskini, baadhi yao wenye nguvu na wengine madhaifu Na Akawafanya baadhi yao ni wahitaji wa wengine ili kuwajaribu kwa hilo, wapate makafiri matajiri kusema, «Ni madhaifu hawa, miongoni mwetu, Mwenyezi Mungu Amewapa neema ya Uislamu?» Kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, si Mjuzi zaidi wa wanaoshukuru neema Yake Akawaafikia kwenye uongofu wa dini Yake |