Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 52 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[الأنعَام: 52]
﴿ولا تطرد الذين يدعون ربهم بالغداة والعشي يريدون وجهه ما عليك من﴾ [الأنعَام: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na usiwatenge, ewe Nabii, kukaa na wewe Waislamu wanyonge wanaomuabudu Mola wao mwanzo wa mchana na mwisho wake, hali wakitaka, kwa matendo yao mema, radhi za Mwenyezi Mungu. Kitu chochote kuhusu hesabu ya maskini hawa hakiko juu yako; hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu. Na si juu yao chochote kuhusu hesabu yako. Basi ukiwatenga , utakuwa ni miongoni mwa wenye kuivuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye kuweka vitu mahali pasipokuwa pake |