×

Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na 6:71 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:71) ayat 71 in Swahili

6:71 Surah Al-An‘am ayat 71 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 71 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿قُلۡ أَنَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعۡقَابِنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِي ٱسۡتَهۡوَتۡهُ ٱلشَّيَٰطِينُ فِي ٱلۡأَرۡضِ حَيۡرَانَ لَهُۥٓ أَصۡحَٰبٞ يَدۡعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلۡهُدَى ٱئۡتِنَاۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۖ وَأُمِرۡنَا لِنُسۡلِمَ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[الأنعَام: 71]

Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل أندعوا من دون الله ما لا ينفعنا ولا يضرنا ونرد على, باللغة السواحيلية

﴿قل أندعوا من دون الله ما لا ينفعنا ولا يضرنا ونرد على﴾ [الأنعَام: 71]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Je, tuabudu, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, masanamu yasionufaisha wala kudhuru? Je, turudi ukafirini baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoza kwenye Uislamu, tukafanana, katika kurudi kwetu ukafirini, na aliyeharibika akili yake kwa kusawazwa na mashetani akapotea njia ardhini na hali yeye ana marafiki wenye akili, wenye Imani, wamwita kwenye njia ya sawa ambayo wao wako akawa anakataa?» Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Uongofu wa Mwenyezi Mungu Aliyenituma mimi ndio uongofu wa haki. Na sote tumeamrishwa tujisalimishe kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Bwana wa vuimbe vyote, kwa kumuabudu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani Yeye Ndiye Mola na Mmiliki wa kila kitu.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek