×

Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! 6:73 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:73) ayat 73 in Swahili

6:73 Surah Al-An‘am ayat 73 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 73 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ ﴾
[الأنعَام: 73]

Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وهو الذي خلق السموات والأرض بالحق ويوم يقول كن فيكون قوله الحق, باللغة السواحيلية

﴿وهو الذي خلق السموات والأرض بالحق ويوم يقول كن فيكون قوله الحق﴾ [الأنعَام: 73]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa pungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kwa haki. Na taja,ewe Mtume, Atakaposema Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, «Kuwa» na ikawa kulingana na amri Yake, kama kupepesa macho au muda mfupi zaidi. Neno lake Ndio haki iliokamilika. Na ni Wake ufalme, Peke Yake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Siku Malaika atakapovuvia Parapanda, mvuvio wa pili ambao, kwa huo, roho zitarudi kwenye miili. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni kwake, Ndiye Anayeyajua yaliyofichika na hisi zenu, enyi watu, mnayoyaona kwa macho yenu. Yeye Ndiye Mwenye hekima, Anayeweka mambo mahali pake, Mtambuzi wa mambo ya viumbe Vyake. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Anayehusika na mambo haya na mengineyo, mwanzo na mwisho, kuanzisha kuumba na ukomo wake. Na Yeye, Peke Yake, Ndiye Ambaye inapasa kwa waja kufuata sheria Yake, kujisalimisha kwa hukumu Yake na kuwa nahamu ya kupata radhi Zake na msamaha Wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek