Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 76 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبٗاۖ قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأٓفِلِينَ ﴾
[الأنعَام: 76]
﴿فلما جن عليه الليل رأى كوكبا قال هذا ربي فلما أفل قال﴾ [الأنعَام: 76]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Giza la usiku lilipomuingilia Ibrāhīm, amani imshukiye, na kumfinika, alijadiliana na watu wake ili kuwathibitishia kuwa dini yao ni ya urongo. Na wao walikuwa wakiabudu nyota. Ibrāhīm, amani imshukiye, aliona nyota, akasema, akiwavuta watu wake, ili awathibitishie tawhīd (upweke wa Mwenyezi Mungu) kihoja, «Hii ni mola wangu.» Nyota ilipozama alisema, «Mimi siwapendi waungu wanaozama.» |