×

Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi 6:91 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:91) ayat 91 in Swahili

6:91 Surah Al-An‘am ayat 91 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 91 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦٓ إِذۡ قَالُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ بَشَرٖ مِّن شَيۡءٖۗ قُلۡ مَنۡ أَنزَلَ ٱلۡكِتَٰبَ ٱلَّذِي جَآءَ بِهِۦ مُوسَىٰ نُورٗا وَهُدٗى لِّلنَّاسِۖ تَجۡعَلُونَهُۥ قَرَاطِيسَ تُبۡدُونَهَا وَتُخۡفُونَ كَثِيرٗاۖ وَعُلِّمۡتُم مَّا لَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنتُمۡ وَلَآ ءَابَآؤُكُمۡۖ قُلِ ٱللَّهُۖ ثُمَّ ذَرۡهُمۡ فِي خَوۡضِهِمۡ يَلۡعَبُونَ ﴾
[الأنعَام: 91]

Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وما قدروا الله حق قدره إذ قالوا ما أنـزل الله على بشر, باللغة السواحيلية

﴿وما قدروا الله حق قدره إذ قالوا ما أنـزل الله على بشر﴾ [الأنعَام: 91]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na hawa washirikina hawakumtukuza Mwenyezi Mungu ipasavyo kumtukuza, kwani walikanusha kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amemteremshia yoyote miongoni mwa binadamu, chochote katika wahyi wake. Waambie, ewe Mtume, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, ni nani aliyeteremsha kitabu alichokuja nacho Mūsā kwa watu wake, kikiwa ni mwangaza kwa watu na mwongozo kwao?» Kisha maneno yakaelekea kwa Mayahudi kwa kuwakemea kwa kusema «Mnakigawanya kitabu hiki kwenye kurasa mbalimbali, nyingine mnazionesha na nyingi katika hizo mnazificha.- Kati ya hizo walizozificha ni maelezo ya sifa za Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na unabii wake.- Pia Mwenyezi Mungu Aliwafundisha, nyinyi Waarabu, Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwenu, ndani yake mna habari ya walio kabla yenu na walio baada yenu na yatakayokuwa baada ya kufa kwenu, habari ambazo hamkuwa mkizijuwa, nyinyi wala wazazi wenu.» Sema, «Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeiteremsha.» Kisha waache hawa wavame na kucheza katika mazungumzo yao ya ubatili
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek