×

Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea 6:99 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:99) ayat 99 in Swahili

6:99 Surah Al-An‘am ayat 99 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 99 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَيۡءٖ فَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهُ خَضِرٗا نُّخۡرِجُ مِنۡهُ حَبّٗا مُّتَرَاكِبٗا وَمِنَ ٱلنَّخۡلِ مِن طَلۡعِهَا قِنۡوَانٞ دَانِيَةٞ وَجَنَّٰتٖ مِّنۡ أَعۡنَابٖ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشۡتَبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٍۗ ٱنظُرُوٓاْ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَيَنۡعِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمۡ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأنعَام: 99]

Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وهو الذي أنـزل من السماء ماء فأخرجنا به نبات كل شيء فأخرجنا, باللغة السواحيلية

﴿وهو الذي أنـزل من السماء ماء فأخرجنا به نبات كل شيء فأخرجنا﴾ [الأنعَام: 99]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za pungufu ni Kwake, Nadiye Aliyetaramsha mvua kutoka kwenye mawingu, Akatoa kwayo mimea ya kila kitu, Akatoa, kutokana na mimea, nafaka na miti mibichi, kisha akatoa kwenye mimea ya nafaka mbegu zilizoshikana, kama masuke ya mahindi, ngano na mpunga. Na Akatoa kutoka kwenye kizao cha mtende, nacho ni kile ambacho karara la tende linachomoza hapo, mitungo ambayo kuitunda ni karibu. Na Akatoa, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, mashamba ya mizabibu. Na Akatoa mizaituni na mikomamanga ambayo majani yake yanafanana na matunda yake yanatafautiana kimaumbile, uatamu na kitabia. Angalieni, enyi watu, matunda ya mimea hii inapotoa mazao na kuiva kwake na kustawi kwake yanapostawi. Hakika katika hayo, enyi watu, kuna dalili ya ukamilifu wa uwezo wa muumba vitu hivi, hekima Yake na rehema Yake kwa watu wenye kumuamini Yeye, Aliyetukuka, na kuzifuata sheria Yake kivitendo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek