Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 100 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلۡجِنَّ وَخَلَقَهُمۡۖ وَخَرَقُواْ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَٰتِۭ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴾
[الأنعَام: 100]
﴿وجعلوا لله شركاء الجن وخلقهم وخرقوا له بنين وبنات بغير علم سبحانه﴾ [الأنعَام: 100]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hawa washirikina wamefanya majini ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, kwa kuitakidi kwao kuwa wao wanalete manufaa au madhara, na hali Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewaumba wao na wanavyoviabudu kutoka kwenye ‘adam ( hali ya kutokuwako). Basi ni Yeye Aliyepwkeka kwa kuumba, Peke Yake, na inapasa Apwekeke kwa kuabudiwa Peke Yake, Asiye na mshirika. Na, kwa kweli, hawa washirikina walisema urongo kumzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, walipomnasibishia Yeye watoto wa kiume na wakike, kwa kutojua kwao sifa Zake za ukamilifu zinazompasa. Ameepuka na kuwa juu ya yale, ambayo walimnasibisha nayo washirikina, ya urongo na uzushi |