Quran with Swahili translation - Surah As-saff ayat 6 - الصَّف - Page - Juz 28
﴿وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ ﴾
[الصَّف: 6]
﴿وإذ قال عيسى ابن مريم يابني إسرائيل إني رسول الله إليكم مصدقا﴾ [الصَّف: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakumbushe ewe Mtume, watu wako pindi Īsā, mwana wa Maryam, alipowaambia watu wake, «Mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu, ni mwenye kusadikisha Taurati iliyokuja kabla yangu na ni mwenye kushuhudilia ukweli wa Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na ni mwenye kulingania watu wamuamini, basi alipowajia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa aya zilizo wazi walisema, «Huu ni uchawi waziwazi.» |