Quran with Swahili translation - Surah As-saff ayat 7 - الصَّف - Page - Juz 28
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[الصَّف: 7]
﴿ومن أظلم ممن افترى على الله الكذب وهو يدعى إلى الإسلام والله﴾ [الصَّف: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi na adui zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo na akamfanya kuwa ana washirika wa kuabudiwa, na hali yeye anaitwa aingie kwenye Uislamu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa ibada. Na Mwenyezi Mungu Hawaafikii, wale waliozidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na kukanusha, kwenye njia ambayo ndani yake kuna kufaulu kwao |