Quran with Swahili translation - Surah At-Tahrim ayat 3 - التَّحرِيم - Page - Juz 28
﴿وَإِذۡ أَسَرَّ ٱلنَّبِيُّ إِلَىٰ بَعۡضِ أَزۡوَٰجِهِۦ حَدِيثٗا فَلَمَّا نَبَّأَتۡ بِهِۦ وَأَظۡهَرَهُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ عَرَّفَ بَعۡضَهُۥ وَأَعۡرَضَ عَنۢ بَعۡضٖۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِۦ قَالَتۡ مَنۡ أَنۢبَأَكَ هَٰذَاۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡخَبِيرُ ﴾
[التَّحرِيم: 3]
﴿وإذ أسر النبي إلى بعض أزواجه حديثا فلما نبأت به وأظهره الله﴾ [التَّحرِيم: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pindi Mtume alipompa siri mke wake Hafsah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, ya mazungumzo fulani, na yeye alipomwambia maneno hayo mke mwenzake 'Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, na Mwenyezi Mungu Akamjulisha Mtume Wake kuwa mkewe ameitoa siri yake, alimjulisha Hafsah sehemu ya maneno aliyoyatoa na akayanyamazia mengine asimwambie kwa kuchunga heshima. Basi Mtume alipomwambia Hafsah yale mazungumzo aliyoyatangaza, alisema huyo mke, «Ni nani aliyekwambia maneno hayo?» Akasema Mtume, «Aliyenambia hayo ni Mwenyezi Mungu, Aliye Mwingi wa ujuzi na utambuzi, Ambaye hakifichamani Kwake chenye kujificha chochote |