Quran with Swahili translation - Surah At-Tahrim ayat 8 - التَّحرِيم - Page - Juz 28
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ تُوبُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ تَوۡبَةٗ نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيُدۡخِلَكُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ يَوۡمَ لَا يُخۡزِي ٱللَّهُ ٱلنَّبِيَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥۖ نُورُهُمۡ يَسۡعَىٰ بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَبِأَيۡمَٰنِهِمۡ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتۡمِمۡ لَنَا نُورَنَا وَٱغۡفِرۡ لَنَآۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ﴾
[التَّحرِيم: 8]
﴿ياأيها الذين آمنوا توبوا إلى الله توبة نصوحا عسى ربكم أن يكفر﴾ [التَّحرِيم: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Acheni madhambi yenu na mrudi kwenye kumtii Mwenyezi Mungu, kurudi kwa mwisho kusikokuwa na ufanyaji maasia tena kwa kutarajia Mola wenu Awafutie maovu ya matendo yenu na Awaingize kwenye mabustani ya Peponi ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito ya maji, Siku ambayo Mwenyezi Mungu Hatamfedhehi Nabii na walioamini pamoja naye wala hatawatesa, bali Atavipandisha juu vyeo vyao. Nuru ya watu hawa itakuwa inatembea mbele yao na kuliani mwao huku wakisema, «Mola wetu! Tukamilishie sisi nuru yetu mpaka tuvuke Ṣirāṭ na tuongoke njia ya kwenda Peponi, na utusamehe na uyatupilie mbali madhambi yetu na uyasitiri, kwani wewe Kwa hakika ni Muweza juu ya kila kitu.» |