Quran with Swahili translation - Surah Al-Mulk ayat 8 - المُلك - Page - Juz 29
﴿تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۖ كُلَّمَآ أُلۡقِيَ فِيهَا فَوۡجٞ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُهَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٞ ﴾
[المُلك: 8]
﴿تكاد تميز من الغيظ كلما ألقي فيها فوج سألهم خزنتها ألم يأتكم﴾ [المُلك: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr unakaribia huo moto wa Jahanamu kurarukararuka kwa ukali wa hasira ulizonazo juu ya wakanushaji. Kila linapotiwa humo kundi la watu, wale wawakilishi wa kusimamia mambo ya huo moto wa Jahanamu watawauliza kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia: Je kwani hakuwajia nyinyi, huko duniani, mjumbe wa kuwatahadharisha na adhabu hii ambayo nyinyi mmo ndani yake |