Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 116 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ ﴾
[الأعرَاف: 116]
﴿قال ألقوا فلما ألقوا سحروا أعين الناس واسترهبوهم وجاءو بسحر عظيم﴾ [الأعرَاف: 116]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akasema Mūsā kuwaambia wachawi, «Tupeni nyinyi.» Walipotupa kamba na fimbo, waliyaroga macho ya watu yakaona kwamba yale waliyoyafanya ni ya kweli, na hali yalikuwa ni kiinimacho na vitu vya kudhania, na waliwatisha watu vitisho vikali na walikuja na uchawi wa nguvu ulio mwingi |