Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 128 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ ﴾
[الأعرَاف: 128]
﴿قال موسى لقومه استعينوا بالله واصبروا إن الأرض لله يورثها من يشاء﴾ [الأعرَاف: 128]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akasema Mūsā kuwaambia watu wake, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, «Takeni msaada kwa Mwenyezi Mungu Awaokoe na Fir'awn na watu wake, na subirini juu ya shida zinazowapata nyinyi na watoto wenu kutoka kwa Fir 'awn. Kwani ardhi yote ni ya Mwenyezi Mungu Anamrithisha Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwisho mwema ni wa anyemcha Mwenyezi Mungu akafanya maamrisho Yake na akajiepusha na makatazo Yake |