Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 127 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 127]
﴿وقال الملأ من قوم فرعون أتذر موسى وقومه ليفسدوا في الأرض ويذرك﴾ [الأعرَاف: 127]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watukufu na wakubwa miongoni mwa watu wa Fir'awn walisema kumwambia Fir'awn, «Unamuacha Mūsā na watu wake, Wana wa Isrāīl, wawaharibu watu katika nchi ya Misri kwa kuwageuzia dini yao na kuwaletea ibada ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, Asiye na mshirika, na kuacha kukuabudu wewe na kuwaabudu waungu wako?» Fir'awn akasema,»Tutawaua watoto wa kiume wa Wana wa Isrāīl, na tutawaacha watoto wao wa kike waishi ili watumike; na sisi tuko juu yao kwa nguvu za ufalme na mamlaka.» |