Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 131 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿فَإِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡحَسَنَةُ قَالُواْ لَنَا هَٰذِهِۦۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَطَّيَّرُواْ بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓۗ أَلَآ إِنَّمَا طَٰٓئِرُهُمۡ عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 131]
﴿فإذا جاءتهم الحسنة قالوا لنا هذه وإن تصبهم سيئة يطيروا بموسى ومن﴾ [الأعرَاف: 131]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ukiwajia Fir'awn na watu wake urutuba na chakula huwa wakisema, «Hii ni yetu tunayoistahiki.» Na ukiwapata wao ukame na chaka huwa wakiona wameingiliwa na ukorofi na huwa wakisema, «Haya ni kwa sababu ya Mūsā na walio pamoja na yeye.»Jua utanabahi kwamba yanayowapata ya ukame na chaka ni kwa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na makadirio Yake, na ni kwa sababu ya madhambi yao na ukafiri wao. Lakini wengi wa watu wa Fir'awn hawalijui hilo, kwa kuvama kwao kwenye ujinga na upotevu.» |