×

Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya 7:146 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:146) ayat 146 in Swahili

7:146 Surah Al-A‘raf ayat 146 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 146 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿سَأَصۡرِفُ عَنۡ ءَايَٰتِيَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلرُّشۡدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلۡغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ ﴾
[الأعرَاف: 146]

Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: سأصرف عن آياتي الذين يتكبرون في الأرض بغير الحق وإن يروا كل, باللغة السواحيلية

﴿سأصرف عن آياتي الذين يتكبرون في الأرض بغير الحق وإن يروا كل﴾ [الأعرَاف: 146]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Nitazipotoa nyoyo za wenye kufanya kiburi wakaacha kunitii na wenye kuwafanyia watu kiburi pasi na haki zisizielewe hoja na dalili zinazoonesha ukubwa wangu, sheria yangu na hukumu zangu, wawe hawamsikilizi Mtume yoyote kwa kiburi chao. Na wakiona, hawa wenye kuifanyia Imani kiburi, kila alama hawaiyamini, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na kupingana kwao na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Wakiiyona njia ya uongofu hawaifanyi ni njia, na wakiiyona njia ya upotevu wanaifanya kuwa ni njia na ni dini. Hayo ni kwa sababu ya kukanusha kwao aya za Mwenyezi Mungu na kughafilika kwao kuziangalia na kuyatia akilini maana yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek