×

Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. 7:145 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:145) ayat 145 in Swahili

7:145 Surah Al-A‘raf ayat 145 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 145 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ ﴾
[الأعرَاف: 145]

Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وكتبنا له في الألواح من كل شيء موعظة وتفصيلا لكل شيء فخذها, باللغة السواحيلية

﴿وكتبنا له في الألواح من كل شيء موعظة وتفصيلا لكل شيء فخذها﴾ [الأعرَاف: 145]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na tulimuandikia Mūsā katika Taurati mawaidha ya kila anachokihitajia katika hukumu za Dini yake, ili yapatikane makemeo na mazingatio, na maelezo yanayofafanua mambo ambayo walikalifishwa nayo ya halali na ya haramu, maamrisho na makatazo, visa, mambo ya itikadi, habari na mambo yasiyoonekana. Mwenyezi Mungu Alimwambia, «Basi yashike kwa nguvu.» Yaani, ishike Taurati kwa kwa bidii na hima. «Na uwaamrishe watu wako wazitumie sheria za Mwenyezi Mungu zilizomo humo. Hakika mwenye kushirikisha miongoni mwao na wengineo, mimi nitamuonesha huko Akhera nyumba ya waasi, nayo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ambao Ameutayarisha kwa maadui Wake waliyotoka nje ya utiifu Wake.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek