Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 162 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَظۡلِمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 162]
﴿فبدل الذين ظلموا منهم قولا غير الذي قيل لهم فأرسلنا عليهم رجزا﴾ [الأعرَاف: 162]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waliomkanusha Mwenyezi Mungu kati yao waliligeuza neno ambalo Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha waliseme, wakaingia mlangoni wakijikokota kwa matako yao na wakasema, «habbah fī sha'rah» (mbegu kwenye unywele), hapo tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni, tukawaangamiza kwayo, kwa sababu ya udhalimu wao na uasi wao |