Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 172 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ ﴾
[الأعرَاف: 172]
﴿وإذ أخذ ربك من بني آدم من ظهورهم ذريتهم وأشهدهم على أنفسهم﴾ [الأعرَاف: 172]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ādam kutoka kwenye migongo ya baba zao, Akawathibitishia upweke Wake kwa kuwatia tabia ya kimaumbile kwamba Yeye ni Mola wao, ni Muumba wao na ni Mmiliki wao; wakamkubalia hilo kwa kuchelea wasije kukanusha Siku ya Kiyama wasikubali chochote katika hilo na wasije wakadai kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu haijasimama kwao na wala hawajui chochote juu yake, bali wao walikuwa wameghafilika na hilo |