Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 171 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿۞ وَإِذۡ نَتَقۡنَا ٱلۡجَبَلَ فَوۡقَهُمۡ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٞ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُۥ وَاقِعُۢ بِهِمۡ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ﴾
[الأعرَاف: 171]
﴿وإذ نتقنا الجبل فوقهم كأنه ظلة وظنوا أنه واقع بهم خذوا ما﴾ [الأعرَاف: 171]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipoliinua jabali juu ya Wana wa Isrāīl likawa kama kwamba ni kiwingu kinachowafinika, wakawa na yakini kuwa kitawaangukia iwapo hawatazikubali hukumu zilizomo kwenye Taurati, na tukawaambia,»Chukueni tulichowapa kwa nguvu.» Yaani, fuateni kivitendo tulichowapa kwa bidii yenu, na yakumbukeni yaliyomo kwenye Kitabu chetu ya ahadi na masharti tuliyoyachukuwa kwenu kwamba mtayatekeleza yaliyomo ndani yake, ili mumche Mola wenu mpate kuokoka na mateso Yake |