×

Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa 7:187 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:187) ayat 187 in Swahili

7:187 Surah Al-A‘raf ayat 187 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 187 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 187]

Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini aghlabu ya watu hawajui

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يسألونك عن الساعة أيان مرساها قل إنما علمها عند ربي لا يجليها, باللغة السواحيلية

﴿يسألونك عن الساعة أيان مرساها قل إنما علمها عند ربي لا يجليها﴾ [الأعرَاف: 187]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanakuuliza, ewe Mtume, makafiri wa Makkah kuhusu Kiyama: kusimama kwake ni lini? Waambie, elimu ya kusimama kwake iko kwa Mwenyezi Mungu, haitoi nje isipokuwa Yeye, imekuwa nzito kuijua na imefichika kwa watu wa mbinguni na ardhini. Hakuna Malaika aliyekaribishwa wala Mtume aliyetumilizwa anayejua wakati wa kusimama kwake. Hakiji isipokuwa kwa ghafla. Hawa watu wanakuuliza kuhusu hiko Kiyama kama kwamba wewe una pupa la kukijua, una bidii sana ya kukiuliza. Waambie, «Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Anayajua yaliyofichika kwenye mbingu na ardhi. Lakini wengi wa watu hawajui kwamba hilo hakuna anayelijua isipokuwa Mwenyezi Mungu.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek