×

Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na 7:43 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:43) ayat 43 in Swahili

7:43 Surah Al-A‘raf ayat 43 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 43 - الأعرَاف - Page - Juz 8

﴿وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلّٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي هَدَىٰنَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهۡتَدِيَ لَوۡلَآ أَنۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُۖ لَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّۖ وَنُودُوٓاْ أَن تِلۡكُمُ ٱلۡجَنَّةُ أُورِثۡتُمُوهَا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[الأعرَاف: 43]

Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na watasema: Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuhidi kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutuhidi. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta Haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Pepo mliyo rithishwa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyafanya

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ونـزعنا ما في صدورهم من غل تجري من تحتهم الأنهار وقالوا الحمد, باللغة السواحيلية

﴿ونـزعنا ما في صدورهم من غل تجري من تحتهم الأنهار وقالوا الحمد﴾ [الأعرَاف: 43]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ataziondoa chuki na mafundo ndani ya vifua vya watu wa Peponi. Na miongoni mwa kukamilika neema zao ni kwamba mito ya maji itakuwa ikipita chini yao. Na watasema watu wa Peponi pindi watakapoingia humo, «Shukrani ni za Mwenyezi Mungu Aliyetuafikia kufanya vitendo vyema ambavyo vimetupatia starehe hizi ambazo tuko nazo. Na hatukuwa tuna uwezo wa kuifuata njia iliyolingana sawa kama si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kutuongoza kufuata njia hii na kutuwezesha kukita juu yake. Mitume wa Mola wetu wametuletea habari za ukweli za ahadi njema kwa wenye kumtii na za kuwaonya wenye kumuasi. Na wataitwa kwa kupongezwa na kukirimiwa waambiwe, «Hiyo ndiyo pepo Mwenyezi Mungu Aliyowapa ni urathi kwa rehema Zake na kwa mliyoyatanguliza ya Imani na matendo mema.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek