×

Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi 7:54 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:54) ayat 54 in Swahili

7:54 Surah Al-A‘raf ayat 54 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 54 - الأعرَاف - Page - Juz 8

﴿إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۭ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[الأعرَاف: 54]

Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن ربكم الله الذي خلق السموات والأرض في ستة أيام ثم استوى, باللغة السواحيلية

﴿إن ربكم الله الذي خلق السموات والأرض في ستة أيام ثم استوى﴾ [الأعرَاف: 54]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika Mola wenu, enyi watu, ni Yule Aliyeanzisha mbingu na ardhi kutoka kwenye 'adam (hali ya kutokuwako) kwa Siku Sita, kisha Akalingana, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, juu ya 'Arsh, -yaani : Alikuwa juu- mlingano unaonasibiana na utukufu na ukubwa Wake. Yeye , kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anauingiza usiku kwenye mchana ukaufinika mpaka mwangaza wake ukaondoka, na Anauingiza usiku kwenye mchana mpaka giza lake likaondoka. Na daima kila mojawapo, kati ya viwili hivyi, kinafuata kingine kwa kasi. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba jua, mwezi na nyota zikiwa zinamtii Yeye, Anazipelekesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vile Anavyotaka, nazo ni miongoni mwa alama kubwa za Mwenyezi Mungu. Jua utanabahi kwamba ni wake Yeye, kutakasika na sifa za upungufu na kutukuka ni Kwake, uumbaji wote, na ni Yake Yeye amri yote. Ametukuka Mwenyezi Mungu, umeendelea ukuu Wake na Ameepukana na kila upungufu, Bwana wa viumbe wote
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek