Quran with Swahili translation - Surah Al-Jinn ayat 28 - الجِن - Page - Juz 29
﴿لِّيَعۡلَمَ أَن قَدۡ أَبۡلَغُواْ رِسَٰلَٰتِ رَبِّهِمۡ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيۡهِمۡ وَأَحۡصَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ عَدَدَۢا ﴾
[الجِن: 28]
﴿ليعلم أن قد أبلغوا رسالات ربهم وأحاط بما لديهم وأحصى كل شيء﴾ [الجِن: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ili Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ajue kwamba Mitume kabla yake walikuwa kwenye hali kama yake ya ufikishaji haki na ukweli, na kwamba yeye atalindwa kutokana na majini kama walivyolindwa wao, na kwamba Mwenyezi Mungu, ujuzi Wake umeyazunguka mambo yao waliyonayo ya nje na ya ndani, miongoni mwa sheria na hukumu na mengineyo, hakuna chochote kinachompita katika hayo, na kwamba Yeye Amekidhibiti kila kitu kwa hesabu, hakuna chochote kinachofichamana Kwake |