Quran with Swahili translation - Surah Al-Insan ayat 29 - الإنسَان - Page - Juz 29
﴿إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا ﴾
[الإنسَان: 29]
﴿إن هذه تذكرة فمن شاء اتخذ إلى ربه سبيلا﴾ [الإنسَان: 29]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye kujitakia wema nafsi yake ya duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu itakayomfikisha kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake |