Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 1 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَنفَالِۖ قُلِ ٱلۡأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَصۡلِحُواْ ذَاتَ بَيۡنِكُمۡۖ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ﴾
[الأنفَال: 1]
﴿يسألونك عن الأنفال قل الأنفال لله والرسول فاتقوا الله وأصلحوا ذات بينكم﴾ [الأنفَال: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Masahaba Zako wanakuuliza, ewe Nabii, kuhusu ngawira siku ya Badr: utawagawia vipi? Waambie, «Jambo lake limeachiwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake» Mtume ndiye mwenye kusimamia ugawaji wake kwa amri ya Mola wake. Basi jikingeni na mateso ya Mwenyezi Mungu wala msithubutu kumuasi, na muache kubishana na kuteta kwa sababu ya mali, na mzitengeneze hali zenu, na mjilazimishe utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake iwapo nyinyi ni Waumini, kwani Imani inapelekea kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake |