Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 12 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿إِذۡ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ أَنِّي مَعَكُمۡ فَثَبِّتُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ سَأُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ فَٱضۡرِبُواْ فَوۡقَ ٱلۡأَعۡنَاقِ وَٱضۡرِبُواْ مِنۡهُمۡ كُلَّ بَنَانٖ ﴾
[الأنفَال: 12]
﴿إذ يوحي ربك إلى الملائكة أني معكم فثبتوا الذين آمنوا سألقي في﴾ [الأنفَال: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Pindi Mola wako, ewe Nabii, Alipowapelekea wahyi Malaika ambao Mwenyezi Mungu Aliwasaidia nao Waislamu katika vita vya Badr, «Mimi nipo na nyinyi, nawasaidia na kuwahami, watieni hima wale walioamini, nitaweka kwenye nyoyo za waliokanusha kicho kingi, unyonge na utwevu.» Vipigeni, enyi Waumini, vichwa vya makafiri na wapigeni wao kila ncha na kila kiungo |