Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 11 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿إِذۡ يُغَشِّيكُمُ ٱلنُّعَاسَ أَمَنَةٗ مِّنۡهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ لِّيُطَهِّرَكُم بِهِۦ وَيُذۡهِبَ عَنكُمۡ رِجۡزَ ٱلشَّيۡطَٰنِ وَلِيَرۡبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمۡ وَيُثَبِّتَ بِهِ ٱلۡأَقۡدَامَ ﴾
[الأنفَال: 11]
﴿إذ يغشيكم النعاس أمنة منه وينـزل عليكم من السماء ماء ليطهركم به﴾ [الأنفَال: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kumbukeni pindi Mwenyezi Mungu Alipowatia usingizi, ili kuwapa hisia ya amani ya kutoogopa kwamba adui yenu atawashinda, na kuwateremshia kutoka mawinguni maji safi, ili mjisafishe kwayo na uchafu wa nje na Awaondolee, ndani, wasiwasi na mawazo yanayoletwa na Shetani, na ili Aziimarishe nyoyo zenu kwa kuvumilia kwenye vita, na ili nyayo za Waumini ziwe thabiti zisiteleze kwa kuifanya ngumu ardhi ya mchanga kwa mvua hiyo |