Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 17 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿فَلَمۡ تَقۡتُلُوهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمۡۚ وَمَا رَمَيۡتَ إِذۡ رَمَيۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِيُبۡلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡهُ بَلَآءً حَسَنًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ﴾
[الأنفَال: 17]
﴿فلم تقتلوهم ولكن الله قتلهم وما رميت إذ رميت ولكن الله رمى﴾ [الأنفَال: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Nyinyi, enyi Waumini, hamukuwaua washirikina siku ya Badr, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Aliwaua, kwa kuwa Aliwasaidia nyinyi kufanya hilo. Na hukurusha uliporusha, ewe Nabii, lakini ni Mwenyezi Mungu Aliyerusha, kwa kuwa Alikifikisha kile ulichokirusha kwenye nyuso za washirikina; na ili Mwenyezi Mungu Awafanyie mtihani wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Awafikishe kwa sababu ya jihadi kwenye daraja za juu, na Awajulisha wao neema Zake kwao wapate kumshukuru, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hilo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa dua zenu na maneno yenu mliyoyaficha na mliyoyafanya waziwazi, ni Mjuzi wa yenye nafuu kwa waja Wake |