Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 22 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿۞ إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلصُّمُّ ٱلۡبُكۡمُ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ ﴾
[الأنفَال: 22]
﴿إن شر الدواب عند الله الصم البكم الذين لا يعقلون﴾ [الأنفَال: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika waovu zaidi wa wanaotembea kwenye ardhi, miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu, mbele ya Mwenyezi Mungu ni viziwi ambao masikio yao yamezibana kutoisikia haki wakawa hawasikii, mabubu ambao ndimi zao zimeshikwa kutoitamka haki wakawa hawatamki. Hawa ndio wale wasioelewa maamrisho na makatazo yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu |