Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 21 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ ﴾
[الأنفَال: 21]
﴿ولا تكونوا كالذين قالوا سمعنا وهم لا يسمعون﴾ [الأنفَال: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msiwe, enyi Waumini, katika kwenda kinyume kwenu na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, rehema na amani zimshukiye, ni kama washirikina na wanafiki ambao wakisikia Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinasomwa kwao huwa wakisema, «Tumesikia kwa masikio yetu,» na hali wao kwa hakika hawayazingatii wanayoyasikia wala hawayatii akilini |