Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 25 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿وَٱتَّقُواْ فِتۡنَةٗ لَّا تُصِيبَنَّ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمۡ خَآصَّةٗۖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[الأنفَال: 25]
﴿واتقوا فتنة لا تصيبن الذين ظلموا منكم خاصة واعلموا أن الله شديد﴾ [الأنفَال: 25]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na jihadharini, enyi Waumini, na mtihani na mkasa yenye kuwaenea waliofanya makosa na wasiofanya, hawahusishwi nayo wenye maasia wala aliyefanya dhambi; bali yanawapata watu wema pamoja nao iwapo wanaweza kukataza udhalimu wasiukataze. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa mateso kwa mwenye kwenda kinyume na maamrisho Yake na makatazo Yake |