×

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la 8:24 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Anfal ⮕ (8:24) ayat 24 in Swahili

8:24 Surah Al-Anfal ayat 24 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 24 - الأنفَال - Page - Juz 9

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمۡ لِمَا يُحۡيِيكُمۡۖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَحُولُ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَقَلۡبِهِۦ وَأَنَّهُۥٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ ﴾
[الأنفَال: 24]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا استجيبوا لله وللرسول إذا دعاكم لما يحييكم واعلموا أن, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا استجيبوا لله وللرسول إذا دعاكم لما يحييكم واعلموا أن﴾ [الأنفَال: 24]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muhammad kuwa ni Nabii na ni Mtume, Itikieni mwito wa Mwenyezi Mungu na wa Mtume kwa kumtii awaitapo kwenye haki yenye kuwapa uhai. Kwani katika kuitikia mwito huo kunatengeneza maisha yenu katika ulimwengu na Akhera. Na mjue, enyi Waumini, kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Mwenye kuendesha kila kitu na Ndiye Muweza, Anaingilia kati baina ya mtu na kile ambacho moyo wake unakitamani. Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuitikiwa Akiwaita, kwani mamlaka ya kila kitu yako mkononi Mwake. Na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwa Siku isiyo na shaka, ambapo kila mmoja atalipwa kwa analostahili kulipwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek