Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 48 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿وَإِذۡ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلۡيَوۡمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّي جَارٞ لَّكُمۡۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلۡفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكُمۡ إِنِّيٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوۡنَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[الأنفَال: 48]
﴿وإذ زين لهم الشيطان أعمالهم وقال لا غالب لكم اليوم من الناس﴾ [الأنفَال: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbukeni pindi Shetani Alipowapambia washirikina yale waliyoyajia na waliyoyakusudia na akawaambia, «Hamuna yoyote Atakayewashinda leo, na mimi ni msaidizi wenu.» Basi yalipopambana makundi mawili: washirikina wakiwa pamoja na Shetani, na Waislamu wakiwa pamoja na Malaika, alirudi nyuma Shetani akaienda zake na akasema kuwaambia washirikina, «Mimi ni mwenye kujitenga na nyinyi; mimi nawaona Malaika msiowaona waliokuja kuwasaidia Waislamu. Hakika mimi namuogopa Mwenyezi Mungu.» Basi akawaacha na akajitenga nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa mateso kwa aliomuasi na asitubiye toba ya kidhati |