Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 74 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ حَقّٗاۚ لَّهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ ﴾
[الأنفَال: 74]
﴿والذين آمنوا وهاجروا وجاهدوا في سبيل الله والذين آووا ونصروا أولئك هم﴾ [الأنفَال: 74]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wakaacha majumba yao wakaelekea Nyumba ya Uislamu au kwenye nchi ambayo ndani yake watapata utulivu wa kumuabudu Mola wao, wakapigana jihadi kwa kulikuza neno la Mwenyezi Mungu, na wale waliowahami ndugu zao Muhājirūn, wakawapa Makao na wakawaliwaza kwa mali na kwa kuwapa nguvu. Hao basi ndio Waumini wakweli kidhati. Watapata msamaha wa madhambi yao na riziki njema iliyo kunjufu katika mabustani ya Pepo ya starehe |