Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 75 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ مَعَكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ مِنكُمۡۚ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ ﴾
[الأنفَال: 75]
﴿والذين آمنوا من بعد وهاجروا وجاهدوا معكم فأولئك منكم وأولو الأرحام بعضهم﴾ [الأنفَال: 75]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale walioamini, baada ya hawa Muhājirūn na Anṣār, wakagura na wakapigana jihadi pamoja na nyinyi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hao ni katika nyinyi, enyi Waumini; wana haki mlizonazo nyinyi na wana majukumu mliyonayo. Na wenye ujamaa, kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu, baadhi yao wanapewa kipaumbele kwa wengine katika kurithiana kuliko Waislamu wa kawaida. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi, Anayajua yanayowafaa waja Wake kuhusu kurithiana wao kwa wao kwa ujamaa na nasaba na kutorithiana kwa mapatano ya kujihami na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yaliyokuwa mwanzo wa Uislamu |