Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 101 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَمِمَّنۡ حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مُنَٰفِقُونَۖ وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ مَرَدُواْ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعۡلَمُهُمۡۖ نَحۡنُ نَعۡلَمُهُمۡۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيۡنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٖ ﴾
[التوبَة: 101]
﴿وممن حولكم من الأعراب منافقون ومن أهل المدينة مردوا على النفاق لا﴾ [التوبَة: 101]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa watu ambao wako pambizoni mwa Madina kuna Mabedui wanafiki, na miongoni mwa watu wa Madina pia kuna wanafiki waliojikita kwenye unafiki na kuzidi kuendelea nao kwa kupita mipaka katika uasi, kwa namna ambayo yanafichamana kwako, ewe Mtume, mambo yao. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kwa kuuawa na kutekwa na kukashifiwa duniani, na kwa adhabu ya kaburi baada ya kufa, kisha watapelekwa, Siku ya Kiyama, kwenye adhabu kubwa ndani ya Moto wa Jahanamu |