Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 102 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَءَاخَرُونَ ٱعۡتَرَفُواْ بِذُنُوبِهِمۡ خَلَطُواْ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴾
[التوبَة: 102]
﴿وآخرون اعترفوا بذنوبهم خلطوا عملا صالحا وآخر سيئا عسى الله أن يتوب﴾ [التوبَة: 102]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wengine wa Madina na walio pambizoni mwake, walikubali makosa yao, wakajuta na wakatubia kwa hayo, walichanganya matendo mazuri, nayo ni kutubia, kujuta, kukubali makosa na mengineyo miongoni mwa matendo mema, kwa mengine mabaya, nayo ni kujikalia nyuma kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na mengineyo miongoni mwa matendo mabaya. Basi hao yatarajiwa Mwenyezi Mungu Awaelekeze kutubia na aikubali toba yao kutoka kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye kuwarehemu |