Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 112 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿ٱلتَّٰٓئِبُونَ ٱلۡعَٰبِدُونَ ٱلۡحَٰمِدُونَ ٱلسَّٰٓئِحُونَ ٱلرَّٰكِعُونَ ٱلسَّٰجِدُونَ ٱلۡأٓمِرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡحَٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[التوبَة: 112]
﴿التائبون العابدون الحامدون السائحون الراكعون الساجدون الآمرون بالمعروف والناهون عن المنكر والحافظون﴾ [التوبَة: 112]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa sifa za Waumini hawa waliopewa bishara njema ya kuingia Peponi ni kwamba wao ndio wanaotubia, wenye kuondoka kwenye yale ambayo Mwenyezi Mungu Ameyakataza kwenda kwenye yale ambayo Mwenyezi Mungu Anayapenda na Anayaridhia, wale waliomtakasia ibada Mwenyezi Mungu Peke Yake na wakapindana katika kumtii, wale wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote yale ambayo Aliwatahini nayo ya uzuri au ubaya, wenye kufunga, wenye kurukuu katika swala zao, wenye kusujudu katika hizo, wale ambao wanawaamrisha watu kila lile ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameliamrisha na wanawakataza kila lile ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamelikataza, wenye kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu, wenye kumalizikia kwenye kufuata amri Yake na kuepuka katazo Lake, wenye kusimama imara katika kumtii na wenye kukomea pale penye mipaka Yake. Na wape bishara njema, ewe Nabii, waumini hawa waliosifika na sifa hizi ya radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo Yake |