Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 113 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن يَسۡتَغۡفِرُواْ لِلۡمُشۡرِكِينَ وَلَوۡ كَانُوٓاْ أُوْلِي قُرۡبَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ ﴾
[التوبَة: 113]
﴿ما كان للنبي والذين آمنوا أن يستغفروا للمشركين ولو كانوا أولي قربى﴾ [التوبَة: 113]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haifai kwa Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina, hata kama ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwa imefunuka waziwazi kwamba wao ni watu wa Moto wa Jah(Im, kwa kufa kwao katika hali ya ushirikina. Na Mwenyezi Mungu Hawasamehe washirikina, kama alivyosema Aliyetukuka, «Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe Ashirikishwapo» na kama Alivyosema Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Hakika yule anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Ashamharimishia Pepo») |