Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 111 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿۞ إِنَّ ٱللَّهَ ٱشۡتَرَىٰ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَنفُسَهُمۡ وَأَمۡوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلۡجَنَّةَۚ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقۡتُلُونَ وَيُقۡتَلُونَۖ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ وَٱلۡقُرۡءَانِۚ وَمَنۡ أَوۡفَىٰ بِعَهۡدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِۚ فَٱسۡتَبۡشِرُواْ بِبَيۡعِكُمُ ٱلَّذِي بَايَعۡتُم بِهِۦۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ﴾
[التوبَة: 111]
﴿إن الله اشترى من المؤمنين أنفسهم وأموالهم بأن لهم الجنة يقاتلون في﴾ [التوبَة: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mwenyezi Mungu Amenunua kutoka kwa Waumini, nafsi zao na kuwapa wao , badala yake, Pepo na yale Aliyoyatayarisha ya starahe humo ndani, kwa kutoa kwao nafsi zao na mali zao katika kupigana jihadi na maadui wake kwa ajili ya kulitukuza neno Lake na kuidhihirisha dini Yake, wakaua na wakauawa. Hiyo ikiwa ni ahadi juu ya Mwenyezi Mungu iliyothibiti ndani ya Taurati iliyoteremshwa kwa Mūsā, amani imshukiye, na Injili iliyoteremshwa kwa ‘Īsā, amani imshukiye, na Qur’ani iliyoteremshwa kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye. Na hakuna yoyote mwenye utekelezaji zaidi wa ahadi Yake kuliko Mwenyezi Mungu, kwa yule aliyetimiza ahadi yake kwa Mwenyezi Mungu. Basi onesheni furaha, enyi Waumini, kwa biashara yenu mliyoifanya na Mwenyezi Mungu na kwa ahadi Yake, ya Pepo na Radhi, kwenu. Na mapatano hayo ya biashara ndiyo kufaulu kukubwa |