Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 114 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَمَا كَانَ ٱسۡتِغۡفَارُ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوۡعِدَةٖ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوّٞ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنۡهُۚ إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٞ ﴾
[التوبَة: 114]
﴿وما كان استغفار إبراهيم لأبيه إلا عن موعدة وعدها إياه فلما تبين﴾ [التوبَة: 114]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hakukuwa kwa Ibrāhīm kule kumuombea msamaha babake mshirikina isipokuwa ni yatokana na ahadi aliyeitoa kwake, nayo ni neno lake, «Nitakuombea msamaha Mola wangu, kwani Yeye kwangu mimi Ana ukarimu mwingi.» Basi ilipomfunukia wazi Ibrāhīm kwamba babake ni adui wa Mwenyezi Mungu na kwamba kusihi na kukumbusha hakukufaa kitu kwake na kwamba yeye atakufa akiwa kafiri, alimuacha, akaacha kumuombea msamaha na akamwepuka. Kwa kweli, Ibrāhīm, amani imshukiye, ana unyenyekevu mkubwa kwa Mwenyezi Mungu, ni mwenye msamaha mwingi kwa kasoro zinazotoka kwa watu wake |