Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 115 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوۡمَۢا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰهُمۡ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ﴾
[التوبَة: 115]
﴿وما كان الله ليضل قوما بعد إذ هداهم حتى يبين لهم ما﴾ [التوبَة: 115]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi mungu Hakuwa ni Mwenye kuwapoteza watu baada ya kuwapa neema uongofu na taufiki, mpaka awaelezee waziwazi yale ambayo yatawapelekea kumcha Yeye na yale wanayoyahitajia ya misingi ya Dini na tagaa zake. Hakika Mwenyezi Mungu, kwa kila jambo, ni Mjuzi; Amewafundisha nyinyi yale ambayo hamkuwa mkiyajua, amewaelezea waziwazi yale ambayo mtanufaika nayo na Amewasimamishia hoja kwa kuwafikishia ujumbe Wake |