Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 124 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ ﴾
[التوبَة: 124]
﴿وإذا ما أنـزلت سورة فمنهم من يقول أيكم زادته هذه إيمانا فأما﴾ [التوبَة: 124]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pindi Mwenyezi Mungu Aiteremshapo sura, miongoni mwa sura za Qur’ani, kwa Mtume Wake, basi kati ya hawa wanafiki kuna wanaosema, kwa kukanusha na kufanya shere, «Ni nani wenu ambaye sura hii ilimfanya imani yake, kwa Mwenyezi Mungu na aya Zake, iongezeke? Basi wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake,, kule kuteremka sura, kuliwaongezea waolmani kwa kuijua na kuizingatia na kuiamini na kuitumia, na hali wao wanafurahia Imani na yakini Alizowapa Mwenyezi Mungu |