Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 129 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ ﴾
[التوبَة: 129]
﴿فإن تولوا فقل حسبي الله لا إله إلا هو عليه توكلت وهو﴾ [التوبَة: 129]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi washirikina na wanafiki wakikupa mgongo kwa kuacha kukuamini, ewe Mtume, sema kuwaambia, «Mwenye kunitosha ni Mwenyezi Mungu; Ananitosheleza yote yanayonitia hamu, hapana muabudiwa yoyote wa haki isipokuwa Yeye, Kwake yeye nimetegemea na Kwake Yeye nimeyategemeza mambo yangu yote. Kwani Yeye Ndiye Mwenye kuninusuru na Mwenye kunisaidia. Na Yeye Ndiye Mola wa Arsh iliyo kubwa, ambayo ndiyo kiumbe kikubwa kabisa.» |